Ukosefu wa mali,uharibifu wa mazingira,kutotii sheria na ukosefu wa kazi ni moja wapo za shida dhidi dunia yetu inayokumba mwaka huu.Mkutano wa Social Good Summit ni mkutano ambayo huleta watu kutoka nchi tofauti ,sana sana vijana, kujadili na kuswali maswali haya magumu ambayo majawabu yao yametatisha maserekali mengi miaka na mikaka zilizopita.2014

Vijana wamechoka kupumzika au kugojea masuluhisho!Wamechoka kwasababu maserekali haswa maserekli ya Afrika hawataki kuuliza au kuunggana na watu wachanga kurekebisha au kutengeneza nchi haswa  siku zetu za usoni!Viongozi wetu wamekataa kata kata kushuka na kujiuzulu wakati wao wakuondaka ofisini unapofika.Tabia hii ya kutoshirikiana na raia wote na kuenedeleza vipengele shamba unakera na unaudhi sana!

Akina yahe hawakukosea waliponena kuwa afua ni mbili,kufa na kupona!Vijana wamegundua pia kuwa asante ya punda ni mateke na hawata kubali tena kunyamaza au kunyamazishwa na yeyote na wamepata njia injine kupaza sauti zao.Technologia, vyombo vya habari na utumizi wa mtandao umehakikisha sauti za watu kadha wa kadha yanaskizwa.Mkutano huu wa social good summit ni thabiti kuwa ushirikiano wa watu wote na wengi unauzito na unaweza tatua mashaka zetu haraka sana.Mjadali huu wa siku mbili umepanua mafirika zetu sote na sasa viongozi wote  duniani wanaskiza na wanatafakari tunayo nena.

Msemo huu wa kina babu-akishindwa sultani,rai huweza nini? tumetupia mbali!Lakini tusifikiree kuwa hatutapatana na shida kibao siku zijayo!Lakini kweli kwamba umoja ni nguvu na ni haki yetu kuwa wangalifu na kuwacha ndunia yetu nzuri haswa kwasababu ya  watoto wetu na watoto wa watoto wetu pia!Kwa hivyo ni lazima tupambane na dimba zote dunia hii inayakumbana nayo leo!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *